Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo amesema kuwa asilimia kubwa ya madaktari walioko nchini wana msongo wa mawazo kutokana na kazi kubwa ya kuhudumia watu waliyonayo.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waganga Wakuu wa Mikoa katika mkutano wao mkuu wa tatu uliofanyika jijini Dodoma, ambapo amewapongeza kwa kazi yao kubwa, kwani wamekuwa wakijituma na kuwa mstari wa mbele kuokoa maisha ya Watanzania.

Amewapongeza madaktari wa Tanzania kwa kazi kubwa wanayoifanya, ambapo amesema kuwa wanafanya kazi iliyopitiliza kwa kuwatumikia wananchi.

Amesema kuwa madaktari wanafanya kazi kubwa sana ya dhati iliyopitiliza na yeye akimuona mtu anabeza kazi ya madaktari huwa anapata huzuni kubwa.

“Nimefika nilikuwa nawaangalia, wengi sana naona mna ‘stress’ mkutano umepooza, ninachoamini kwamba wengi mnastress lakini stress hizo ni kwa kazi kubwa mnazofanya,” amesema Waziri Jafo.

Aidha, katika pongezi zake Waziri Jafo, ameeleza ni kwa namna gani aliwaona wakijitoa kuhudumia majeruhi wa ajali ya kulipuka kwa tenki la mafuta mkoani Morogoro.

”Mfano mzuri ni wa tukio kubwa la tenki la mafuta kuwaka moto Morogoro,nimefika pale mpaka saa tano za usiku, niliwaona madaktari hata mioyo
imeshakufa ganzi, watu waliokuwa katika hali mbaya, madaktari wakijituma kuwasindikiza Muhimbili,”ameongeza waziri Jafo

 

Watekaji wa 'Mo' bado kitendawili
Video: RC Makonda ashangaa, 'Hata fursa ya Kiswahili nayo hamjaiona?