Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro ametangazwa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, kuwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika siku ya jumapili.

Tume hiyo ya uchaguzi wa Venezuela imemtangaza Rais Nicolas Maduro kuwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika jana Jumapili, ambao ulisusiwa na upinzani ambapo ameshinda kwa zaidi ya asilimia 60.

Aidha, kiwango cha wapiga kura waliojitokeza kilikuwa ni asilimia 46, kitu ambacho wapinzani wamekiita ni kama sherehe ya kumvisha taji dikteta.

Mpinzani pekee aliyesimama dhidi ya rais huyo ni gavana wa zamani wa jimbo, Henri Falcon ambapo amesema kuwa hautambui uchaguzi huo kwa sababu umekumbwa na mizengwe na kutaka zoezi hilo lifanyike upya.

Hata hivyo, baada ya tangazo la tume ya uchaguzi kuhusu ushindi wa Maduro, sherehe kubwa zilianza katika mitaa ya mji mkuu Caracas inayokaliwa na watu wa tabaka la chini.

 

Polisi wapigwa marufuku kula hadharani, kuweka mikono mfukoni
Wanaowekeza fedha kwenye ‘Bitcoins’ watahadharishwa