Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza janga kubwa katika jimbo la West Virginia, kufuatia mafuriko makubwa kuwahi kutokea kwa karne nzima ambapo watu 24 wamefariki.

Kufuatia ombi la Gavana, Earl Ray Tomblin, Rais Obama aliita msaada wa kibinadamu kwa kaunti tatu zilizoathirika vibaya na mafuriko.

Wakaazi sasa watapata misaada ya kujenga nyumba za muda na kukarabati zingine.

Mvua kubwa ya Alhamisi ilisababisha maji kutoka mito na vijito kutenga miji kadhaa.

Mamia ya watu waliokolewa

Rais ampongeza Dj Black Coffee kwa kuwapenya Diamond, Wizkid
Mfereji wa Panama wafunguliwa