Ajali ya Gari iliyotokea mapema hii leo iliyosababishwa na lori la mizigo kugonga gari jingine baada ya mfumo wake wa breki kuharibika, imesababisha kuteketea kwa moto malori matano ya mizigo.

Jeshi la Polisi Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyoteketeza magari matano ya mizigo yaliyokuwepo katika kituo cha forodha cha Rusumo mkoani humo.

Aidha, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ngara, Abeid Maige amesema kuwa polisi wako eneo la tukio hilo kwa ajili ya kuondoa watu katika eneo la tukio, na kwamba taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo zitatolewa hapo baadae.

Hata hivyo inasemekana kuwa Magari hayo yalikuwa katika foleni ya kuingia kwenye kituo cha forodha.

LIVE DODOMA: Taarifa ya Utekelezaji Ilani ya CCM 2016 hadi 2018
Milioni 600 zawaponza, sasa kupisha uchunguzi