Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, John Magufuli amesema tayari Serikali imejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 2020 unakuwa wa amani, huru na wa haki.

Magufuli amesema utakapofika uchaguzi huo, nchi na taasisi mbalimbali zitakaribishwa Tanzania kushuhudia.

Ametoa kauli hiyo jana, Ikulu, Jijini Dar es salaam, alipokutana na mabalozi wanaowaziwakilisha nchi zao Tanzania ili kuwatakia heri ya mwaka mpya 2020.

“Mwaka 2020 mwezi oktoba nchi yetu itafanya uchaguzi mkuu, zoezi la uchaguzi ni muhimu kwa nchi yoyote inayofuata msingi wa demokrasia, Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu utafanyika katika mazingira ya amani, uhuru na haki” alisema Rais Magufuli.

Na kusisitiza kuwa ” Kama ilivyo kawaida yetu wakati ukifika tutazikaribisha nchi na taasisi mbalimbali kuja kuangalia uchaguzi wetu ili kujionea jinsi nchi yetu inavyokomaa katika nyanja ya demokrasia”

TMA yatoa tahadhari upepo mkali na mawimbi Baharini
Video: Kisa mzee Abdul kumuacha Bi Sandra, ''Sijawahi kujuta'', ''Sipendi hiki kwa Diamond''