Rais dkt. John Magufuli ameagiza makontena ya mchanga wa dhahabu ambayo yalizuiwa bandarini yasisafilishwe mwaka 2017 yatafutiwe mteja na yauzwe kwa faida ya kampuni mpya ya Twiga ambayo ni muungano wa hisa za Serikali na za kampuni ya Barrick ili kuanza ukurasa mpya wa biashara.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Ijumaa, Januari 24, 2020 baada ya kutiliwa saini mkataba wa makubaliano baina ya Serikali na kampuni ya madini ya Barrick Ikulu jijini Dar es salaam.

“Namnunuzi namjua, Kwa sasa huyo mnunuzi kama anataka kuja kununua anunue kwasababu tunajua faida itakayo patikana kwaajili ya kampuni yote (Twiga), tuendelee kushirikiana kwaajili ya faida ya pande zote mbili” amesema Rais Magufuli.

Machi 2017, baada ya Rais John Magufuli kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga wenye dhahabu kwenda nje ya nchi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilizuia makontena 262 yenye mchanga huo uliokuwa katika Bandari ya Dar es Salaam kusafirishwa.

Taarifa ya Tume ya Rais ya Uchunguzi chini ya Prof. Mruma iliyowasilishwa Mei 24, 2017 iliyo kuwa inachunguza kiwango cha madini yaliyomo katika makontena ya mchanga (Makinikia) yaliko katika Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yaliyozuiliwa na serikali kusafirishwa kwenda nchi za nje, Imebainisha kuwepo udanganyifu mkubwa kwenye kiwango cha madini yaliyopo kwenye mchanga na thamani halisi.

Katika makontena hayo, kwa kutumia viwango vya wastani thamani ya mtali/madini yote katika makinikia ni TZS bilioni 829.4 na TZS bilioni 1,438.8 kwa kutumia viwango vya juu.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa alikiwa anaumia kuona dhahabu inasombwa na wananchi wanaambiwa ni mchanga wakati katika eneo ambalo kuna migodi wananchi wanaishi maisha duni.

Aidha ameagiza kampuni ya Twiga kuhakikisha wanahifadhi mazingira na kuwasaidia wakazi wa karibu na maeneo ya migodi pale wanapohitaji misaada ya kimaendeleo kama kuwajengea visima vya maji.

Serikali: Hakuna virusi vya Corona Tanzania
Viongozi wa CCM waonywa tabia ya 'Majina mfukoni'