Mahakama Kuu nchini Sierra Leone imesitisha uchaguzi wa marudio wa urais uliokuwa umepangwa kufanyika wiki ijayo baada ya mshindi kutopatikana kwenye uchaguzi wa awali wa Machi 7.

Uamuzi huo wa mahakama umekuja kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Ibrahim Koroma, mwanachama wa chama tawala cha All People’s Congress aliyeeleza kuwa kuna ushahidi wa udanganyifu katika zoezi la awali la upigaji kura.

Taharuki kuhusu kuwepo udanganyifu katika baadhi ya wilaya na malalamiko kuhusu vitisho vya askari wa jeshi la polisi dhidi ya makarani wa Tume ya uchaguzi, vinatajwa kuwa chanzo cha uamuzi huo wa mahakama.

Mgombea wa chama kikuu cha upinzani cha People’s Party, Julius Bio atachuana na mgombea wa chama tawala, Samura Kamara baada ya wawili hao kushindwa kufikisha kura za kutosha vigezo vya kuwa aliyechaguliwa na wengi katika uchaguzi wa kwanza.

Hata hivyo, mahakama hiyo haikutaja tarehe nyingine ya uchaguzi huo wa marudio.

Mchakato huo wa kisiasa nchini humo unaohuishwa na hatua ya rais Ernest Koroma kukubali kuachia madaraka baada ya muda wake kuisha, ni ishara nzuri ya amani nchini humo tangu mauaji ya miaka ya 1990 kufuatia vita ya ndani ya mgogoro wa almasi.

Makumi elfu waandamana Marekani kuhusu sheria ya umiliki silaha
Lissu ambariki Fatme karume kugombea urais TLS