Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Wilaya na Waganga Wakuu wa Mikoa yote nchini kusimamia maadili kwa watumishi wa sekta ya afya, ili fedha zinazotolewa kwenye sekta hiyo ziendane na ubora wa huduma zinazotolewa.

Majaliwa ameyasema wakati akizungumza na Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Ruvuma, kwenye ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Songea na pia kuwaagiza Wakuu wa Wilaya kusimamia upatikanaji wa dawa kutoka Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Busket Fund.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Ruvuma.

Aidha, Waziri Mkuu pia amewataka Wakuu hao wa Wilaya kwa kushirikiana na Wakurugenzi na Maafisa Elimu kusimamia dhamira ya Rais Samia ya kutoa elimu bila malipo kaunzia darasa la awali hadi kidato cha sita, kwa kutembelea shule na kukagua fomu za kujiunga ili kujiridhisha iwapo hakuna michango ya hovyo.

Hata hivyo, Majaliwa ameagiza uwepo wa usimamizi wa shughuli za ustawi wa jamii ikiwemo masuala ya kiuchumi na kwa wafanyabiashara wadogo, wakati na wa kubwa ili kutoa mwelekeo wa ukuaji wa uchumi kwenye jamii.

Singida Big Stars yafafanua usajili wa Kazadi
Rage: Fei Toto asipelekeshwe, aulizwe kwanza