Msanii maarufu wa Bongo Movies, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amefunga ndoa na mchumba wake ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji (CEO), wa EFM na TVE, Francis Antony Ciza maarufu ‘Majizzo’ leo Februari 16, 2021, katika Kanisa Katoliki la Mt. Gasper, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Kupitia picha ambazo zimepostiwa mitandaoni zimeonesha wawili hao wakila kiapo cha kufunga ndoa.

Mahusiano ya Elizabeth Michael Lulu na Majizzo ni ya muda mrefu na walikuwa wote kwenye kipindi ambacho Lulu alikuwa na kesi ya kuua bila kukusudia na kufikia Septemba 30, 2018 Majizzo alimvalisha pete ya uchumba Lulu.

Apigwa risasi kwa kudhaniwa ni nyani
Tozo za fukwe zapigwa marufuku