Mapinduzi ya kisayansi na kiteknolojia duniani yanazidi kuibua mapya huku huduma ya mtandao zinazorahisisha kuiweka dunia kiganjani zinazidi kuwa muhimu kiasi cha kugonga hodi katika makaburi.

Taarifa kutoka nchini Urusi zimeeleza kuwa makaburi matatu maarufu yaliyoko jijini Moscow yanatarajiwa kuwekwa huduma ya mtandao ya ‘Wi-fi’ mapema mwaka 2016.

Kwa mujibu wa tovuti ya Moscow City, makaburi yatakayowekewa huduma hiyo ya Wi-fi ya bure ni ya Novedevichy, Troyekurovskoye na Vagankovo.

Lengo la kuyawekea huduma hiyo makaburi hayo maarufu yanayodaiwa kutembelewa zaidi na wageni wa kitalii kila mwaka ni kurahisisha uwepo wa huduma za mtandao katika eneo hilo la makaburini ili wageni hao wawe na uwezo wa kufuatilia kwenye mtandao taarifa za watu mashuhuri waliozikwa katika eneo hilo.

Kampuni ya Mawasiliano ya YS imeeleza kuwa imejitolea kueweka huduma hiyo ya Wi-fi baada ya kuelezwa kuwa kuna mpango wa kutenga eneo kwa ajili ya watu kutuliza akili wanapokuwa katika maeneo hayo.

Miongoni mwa watu waliozikwa katika eneo hilo ni Mwandishi mashuhuri, Anton Chekhov, rais wa zamani wa Urusi, Boris Yeltsin na Kiongozi wa Usovieti, Nikita Khurushchev.

Kuhusu Matokeo Ya Ubunge Arusha Mjini na Majimbo Mengine Manne
Haki za Binadamu, Utawala Bora Yalaani Hatua za Wakuu wa Wilaya Kuwatupa Selo Watumishi