Wakati Tanzania ikiwa bado inapambana na virusi vya Corona, January Makamba aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ameishauri Serikali kuwa kampuni zinazotengeneza pombe kali zinauwezo wa kutengeneza vitakasa mkono (sanitizers) na kuzijaza sokoni.

Kupitia ukurasa wake wa Tweeter ameandika ujumbe huo ambapo ameeleza hata kiwanda cha sukari cha Mtibwa, Kilombero na TPC wanakozalisha Ethanol, sanitizers zinaweza kuwa rahisi kupatikana na kununua.

“Ndugu Waziri kampuni za pombe kali TBL / TDL (konyagi), Mega (K-Vant) na nyingine zinaweza kuambiwa, kuombwa, kusukumwa kuzalisha pia sanitizers na kuzijaza sokoni. Vile vile kwa mtibwa, kilombero sugar, na TPC , kunakozalisha ethanol Sanitizers zapaswa kuwa rahisi kupata na kununua,”. ameandika Makamba.

Mara baada ya serikali kutoa maelekezo wananchi kutumia vitakasa mikono (Hand sanitizer) kwaajili ya kujilinda na  Virusi Coronabidhaa hizo  zimeanza kuwa adimu nchini huku nyingine zikiuzwa kwa bei juu.

 

Daladala zapigwa marufuku kusimamisha abiria
Video: Kishindo cha Mbowe chamtisha Makonda, Polepole, Maswali magumu vita ya Corona