Leo Julai 13, 2018 Makamu Mwenyekiti NCCR Mageuzi Tanzania Bara, Leticia Ghati Masore ametangaza rasmi kurudi CCM akiwa na wenzake watano akiwemo aliyekuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama hicho, Mchata Mchata.

Uamuzi huo ni kufuatia kwa kile alichodai kuwa vyama vya upinzani vinamkera kwani vimekuwa vikipinga kila kitu hadi yale mazuri.

”Kinachonikera kwenye upinzani ni kupinga kila kitu mpaka mazuri wakati hayo ndio tulikuwa tunayasema na mpaka mwisho hatueleweki tunataka nini, kwa hiyo mtu mzima kama mimi nimeona bora nirudi CCM” amesema Bi Leticia.

Endelea kufuatilia Dar24, tutakujuza zaidi.

Necta yatangaza matokeo kidato cha sita, yatazame hapa
Basata yatetea tozo mpya kwenye sanaa, wasanii walia

Comments

comments