Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda anaendelea kukonga nyoyo za kinamama waliotelekezwa na wanaume waliozaa nao, ambapo leo ametoa ripoti ya idadi ya familia alizoziunganisha na idadi ya watu ambao tayari wamekwisha hudumiwa kisheria.

Amesema mpaka sasa amesuluhisha kesi 205, na kesi hizo zimezaa matunda ambapo watoto 205 wamekubaliwa na wanahudumiwa na baba zao na mama zao kama ambavyo ilitakiwa kuwa mbali na idadi hiyo Makonda ametangaza kuwa ikiwa leo ni siku ya tano tangu kuanza kwa zoezi hilo ameshahudumia wanawake 4000 na bado zoezi linaendelea.

”Leo tumefika siku ya tano, zaidi ya watu 4000 wameshapatiwa huduma kwa hesabu ya jana, na zaidi ya familia  205 maana yake zaidi ya watoto 205 wameondoka kwenye mfumo wa kuwa omba omba sasa wanapatiwa huduma na baba zao na mama zao wakiwa  pamoja” amesema Makonda.

Aidha Makonda ameendelea kumshukuru Mungu kwa ujasiri na uthubutu huo na amesema,

”Moyo wangu unafuraha sana kwasababu nilikuwa natafuta hata mmoja akiwa na furaha jina la Mungu lieendelee kutukuzwa” amemalizia Makonda.

Mbali na kuwa tayari amehudumia idadi hiyo ya kinamama, bado namba ya kinamama ambao hawajahudumiwa ni kubwa na hii inaonyesha ni jinsi gani siku hizi watoto wengi wanalelewa na mzazi mmoja hali ambayo siyo nzuri hasa katika kukuza maadili ya mtoto kutokana na kuwa mtoto anakuwa katika mazingira magumu sana, hivyo akifika umri anaoweza kujitegemea ni rahisi sana kujiingiza katika shughuli hatarishi.

Hata hivyo mbali na kutoa msaada wa kisheria kwa kinamama hao waliotelekezwa Makonda ameamua kumimina neema kwa watoto wao kwa kuwapatia bima ya Afya ya matibabu bure kwa mwaka mzima.

Urusi yaiponda ripoti kuhusu shambulio la silaha za kemikali
UDART yaingia mkataba na TTCL