Mkuu wa Idara ya Ardhi Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam, Paul Mbembela alijikuta akipoteza fahamu muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kuagiza avuliwe madaraka mara moja.

Hali ya ofisa Ardhi huyo ilikuwa mbaya baada ya Makonda kuagiza kuvuliwa madaraka hadharani hivyo kulazimu kukimbizwa katika hospitali ya Amana kwa ajili ya kupatiwa matibabu jijini humo.

Akizungumzia hali ya ofisa Ardhi huyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa ofisa huyo alipata mshtuko kutokana na kauli za vitisho kutoka kwa Makonda, ambapo hadi sasa anaendelea vizuri.

“Walivyomtoa pale ukumbini hali yake ilikuwa mbaya, ikalazimu kumkimbiza katika hospitali ya Amana kwa ajili ya kupatiwa matibabu,”amesema Mjema

Hata hivyo, mbali na Mbembela aliyepoteza fahamu, mtumishi mwingine aliyevuliwa madaraka ni Khamis Songwe ambaye ni Mkuu wa Idara ya Ardhi wilaya ya Ubungo.

Bocco awaita mashabiki uwanja wa Taifa
Video: Mkwara wa Makonda nusura uue, Chadema, Cuf walia hujuma Kinondoni

Comments

comments