Makumi elfu wameandamana leo nchini Marekani wakiunga mkono harakati zilizopewa jina la ‘March For Our Lives’, zenye lengo la kushikiniza sheria kali zaidi kubana umiliki silaha za moto.

Maandamano hayo yanaongozwa na wahanga wa shambulizi la risasi katika shule ya Florida mwezi uliopita ambalo lilichochea hasira zaidi dhidi ya mauaji ya aina hiyo.

Wanafunzi wa shule ya Parkland ya Florida ambapo watu 17 waliuawa Februari 14 mwaka huu, wanatarajiwa kuzungumza kwenye tukio hilo kubwa jijini Washington ambako zaidi ya watu 500,000 wanatarajiwa kuhudhuria na kushiriki maandamano.

Hatua hiyo ni kujaribu kushinikiza kupitishwa kwa sheria mpya za kubana uuzaji wa silaha kwa watu binafsi nchini humo.

Matukio ya kushambuliwa kwa risasi kiholela kwenye maeneo ya mikusanyiko ya watu kama shuleni na vyuoni yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara.

Waandamanaji wameshikilia mabango yenye jumbe mbalimbali zinazoweza kutafsiriwa kama ‘Je, Mimi ninafuata?’ ‘Wito kwa usalama wa binti na vijana wetu’ na ‘Ni muda wa kutenda’.

JWTZ, Polisi, magereza wafanya mazoezi ya pamoja ya utayari
Mahakama yasitisha uchaguzi wa marudio wa urais Sierra Leone