Watu kumi na wawili wamepoteza maisha nchini Nigeria baada ya tenki la mafuta kulipuka mwishoni mwa wiki, kwa mujibu wa taarifa ya polisi.

Tukio hilo limesababisha vifo vya watu kutokana na mlipuko wa matenki ya mafuta nchini humo kufikia mamia ndani ya kipindi cha miaka ya hivi karibuni, kutokana na watu kutoboa matenki hayo kwa lengo la kukusanya mafuta.

“Tumekusanya miili 12 ya watu waliopoteza maisha pamoja na watu 22 waliojeruhiwa vibaya kutokana na kuungua na tumewapeleka hospitalini,” msemaji wa Polisi, Irene Ugbo ameiambia Associated Press jana.

Amesema kuwa mlipuko huo ulitokea Ijumaa jioni katika eneo la Odukpani kwenye jimbo la Cross River.

Baadhi ya mashuhuda waliohojiwa wamedai kuwa idadi kuwa idadi ya waliopoteza maisha wanafikia 60 na kwamba miili mingine haikuchukuliwa na polisi.

Video: Mnyika amvaa Spika Ndugai, Maajabu 8 ya Zanzibar
Shein awakingia kifua JPM, JK kutohudhuria miaka 55 ya mapinduzi ya Zanzibar

Comments

comments