Meneja mtarajiwa wa klabu ya Man Utd, Jose Mourinho ameripotiwa kufikia makubaliano ya awali na uongozi wa klabu hiyo ya Old Trafford ya kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Mourinho alianza kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo ya mjini Manchester mwishoni mwa juma lililopita, na amekubali kupokea mshahara wa Pauni milioni 60 kwa mwaka.

Taarifa hizo zimeeleza kwamba huenda hii leo, pande hizo mbili zikasaini mkataba huo kabla ya kutangazwa kwa Jose Mourinho kama meneja rasmi wa Man Utd.

Jorge Mendes is not in London to hold face-to-face talks with Ed WoodwardJorge Mendes

Wakala wa meneja huyo kutoka nchini Ureno, Jorge Mendes amekua na vikao vya mara kwa mara na mtendaji mkuu wa Man Utd, Ed Woodward, huko jijini London, hatua ambayo imechukuliwa kama kuiva kwa dili la Mourinho kupewa kibarua.

Mourinho mwenye umri wa miaka 53, amekua katika vyombo vya habari kwa muda wa siku kadhaa sasa, akihusishwa na mipango kutaka kujiunga na Man Utd, hasa baada ya kutimuliwa kwa aliyekua meneja Louis Van Gaal  mwanzoni mwa juma hili.

MAJALIWA AKUTANA NA KAGAME, WATANZANIA WAISHIO ZAMBIA - PICHA
Simba Wapendekeza 33, Mayanja Asubiriwa Kuwasilisha Wake