Manchester City, imekua ya klabu ya kwanza kwa England kutinga katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu, baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya mabingwa wa soka kutoka nchini Urusi, Dynamo Kiev.

Man City, imefanya hivyo ikiwa ni mara yake ya kwanza kutinga katika hatua hiyo, kufuatia kujikusanyia ushindi wa jumla wa mabao matatu kwa moja dhidi ya wapinzani wao, ambao walikubali kufungwa nyumbani, majuma mawili yaliyopita.

Hatua hii itakua ni heshima kwa meneja Manuel Pellegrini, ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuthibitika nafasi yake itachukuliwa na Pep Guardiola, anayetokea FC Bayern Munich.

Wakati Man City wakiweka historia ya kutinga kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, beki na nahodha wa klabu hiyo, Vincent Jean Mpoy Kompany, huenda akawa nje ya uwanja kwa siku kadhaa kufuatia kuumia kiazi cha mguu, katika mchezo dhidi ya Dynamo Kiev.

Injury-plagued Vincent Kompany can't hide his disappointment as he hobbles off injured early on

Pellegrini alithibitisha kuumia kwa beki huyo kutoka nchini Ubelgiji, huku akisisitiza kusubiri majibu ya vipimo ambayo yatatoka hii leo ili kujua atakua ameumia kwa kiasi gani.

Hii ni mara ya 14 kwa Kompany kuumia tangu alipojiunga na Man City mwaka 2008 na amecheza michezo 19 kati ya 46 ya msimu huu.

Togo Wakubali Kucheza Mjini Monastir Kwa Idhini Ya CAF
Lowassa adai anawaumiza CCM, awafungukia wanaotaka kufukuzwa kwa ajili yake