Uongozi wa klabu ya Man Utd unajipanga kufanya mazungumzo na mshambuliaji kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic, ili kuangalia uwezekano wa kumuongeza mkataba.

Meneja wa Man Utd Jose Mourinho, amethibitisha mpango huo mbele ya waandishi wa habari, ambapo amesema litakua jambo la faraja kwao kama litafanikiwa.

Ibrahimovic alijiunga na Man Utd baada ya kumaliza mkataba na klabu ya Paris Saint-Germain mwezi Julai, na alikubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35, hajawahi kuzungumza chochote kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba mpya, hivyo mpango wa uongozi wa Man Utd huenda ukawa mgeni kwake.

Ibrahimovic ameshafanikiwa kufunga mabao 17 katika michezo ya michuano yote aliyocheza tangu mwanzoni mwa msimu huu, na kasi hiyo inachukuliwa kama kichocheo kwa viongozi wa Man Utd kuona umuhimu wa kumsainisha mkataba mpya.

Mpaka sasa Ibrahimovic ameshashinda mataji 11 ya ligi za mataifa aliyobahatika kucheza, na anakumbukwa kwa rekodi aliyoiacha katika timu yake ya taifa ya swden ya kufunga mabao 62 katika michezo 116 aliyocheza, kabla ya kutangaza kustaafu baada ya fainali za Euro 2016.

Santi Cazorla Kuhamia Italia?
Real Madrid Kumuharakisha Gareth Bale