Wakati Simba SC wakihaha kurejea katika njia ya furaha na kusaka namna ya kutetea ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo, kwa majirani zao Young Africans wameapa msimu huu ‘PATACHIMBIKA’.

Simba SC imekua na matokeo mabaya katika michezo mitatu iliyopita, ikipoteza dhidi ya Mbeya City na Kagera Sugar kwa kufungwa 1-0, huku ikitoka sare ya 0-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Akizungumza mapema leo Alhamis (Januari 27) kupitia Wasafi FM, Msemaji wa Young Africans Haji Manara amesema msimu huu ni wa furaha kwa Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo.

Amesema Wachezaji wanatambua mchango wa Wanachama na Mashabiki wa Young Africans, hivyo jukumu lao ni kupambana na kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano kupita.

“Wachezaji tumekua tukiwahimiza wapambane kwa ajili ya Mashabiki na Wanachama, hawa watu wamesubiri ubingwa kwa miaka minne, tumewaambia Wachezaji wasahau kuhusu Posho kwa sababu hili suala lipo kwenye mikataba yao, jambo la kwanza ni wao kupambana kwanza na mengine yatakuja yenyewe.”

Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha alama 35, baada ya kucheza michezo 13, ikiwaacha Simba SC kwa tofauti ya alama 10.

Watoto wenye matatizo ya moyo wapata ahueni JKCI
Rais Samia:Tufanye kazi kwa bidii