Mkuu wa Idara ya Habari ya Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC, Haji Manara hatokuwa sehemu ya mashuhuda wa mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho *ASFC* utakaochezwa baadae leo Jumamosi (Julai 25) Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma.

Manara amethibitisha kukwama kuelekea Kigoma akitokea Kigali Rwanda, kwa sababu za mlipuko wa maambukizi ya Corona nchini humo.

Jana Manara aliahidi kufika Kigoma akitokea Rwanda kwa kutumia usafiri wa gari.

Manara ameandika kwenye kurasa zake za Mitandao ya Kijamii: “Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu zikiwemo protocol za Covid 19 nimeshindwa kutoka nilipo kuwahi mechi ya leo Kigoma , na nimejisikia vibaya sana, Lakini kidhati kabisa naamini tutashinda na tutarudi Dar na Kombe letu.

Last week nilisema sioni njia ya Simba kufungwa mara mbili mfululizo na Watani zetu na najua Wachezaji wetu hawawezi kuwa wanyonge twice, ingawa pia natambua anything katika Football linawezekana!!

Kutokuwepo kwangu hakutapunguza wala kutoongeza lolote leo sana sana kuniweka na presha kubwa ya kuangalia kipute hiki katika TV.

Nitaangalia hii mechi nikiwa na Tasbihi nikimswalia Mtume (S.A.W) muda wote wa mchezo na kumtaja Mungu wangu na Inshaallah Kwa jitihada za wachezaji wetu na Rehma zake Allah Tutashinda 🙏🤲”

Vandenbroeck aikataa Simba SC usajili 2021/22
Said El Maamry afariki dunia, kuzikwa leo Dar