Mwenyekiti wa Young Africans, aliyechukua fomu za kutetea nafasi hiyo muda mfupi uliopita jijini Dar es Salam, Yusuf Manji amesema kwamba ameleta wachunguzi kutoka nje wachunguze wanaotaka kumhujumu.

Manji ambaye alichukua fomu sambamba na makamu wake, Clement Sanga amesema wachunguzi hao wanaendelea na kazi yao na watatumbua majipu muda si mrefu na wanaomhujumu watajulikana.

Kwa mujibu wa uongozi wa Young Africans uchaguzi utafanyika Juni 11 na si Juni 25 kama iliyotangazwa na TFF.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji amemvua uanachama Mzee Msumi baada ya kudaiwa kufanya njama na viongozi TFF kuhujumu uchaguzi wa klabu hiyo na kupanga safu yao ya uongozi.

Pia amewasimamisha uanachama wale wote waliochukua fomu za kugombea nafasi za uongozi wa Young Africans kupitia TFF.

Magufuli azungumzia waliotimuliwa UDOM, ashangaa fedha kupelekwa kwa ‘vilaza’
Mabondia Wa Kulipwa Waruhusiwa Kushiriki Olympic