Waziri wa tamaduni nchini Guinea amepiga marufuku maonyesho ya urembo hadi pale vipengee vipya vya maadili vitakapo tangazwa.

Serikali ya Guinea imefika maamuzi hayo kufuatia maonyesho ya urembo baada ya kutawaliwa na mavazi ya bikini yaliyopelekea kuzua shutuma nchini humo.

Warembo wakiwa wamevaa bikini walijipanga mbele ya Waziri mkuu, Mamady Youla siku ya Jumamosi na kasababisha shutuma kwenye mitandao ya kijamii kuwa Waziri mkuu alikuwa akiunga mkono ukahaba.

Serikali pia imesema kuwa imefuta mikataba na waandalizi wa maonyesho hayo ya urembo.

Mb Dogg: Muziki ni kama maisha kuna kupanda na kushuka
Gabriel Jesus Ndio Basi Tena, Kujiuguza Miezi Miwili Hadi Mitatu