Mapadri watatu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Same, wamefariki dunia ndani ya saa 72 na wanatarajiwa kuzikwa Aprili 17, 2018 katika Makaburi ya mapadri jimbo la Same.

Waliofariki wametajwa kuwa ni Padre Ubaldus Kidavuri aliyefariki Aprili 13, 2018, Padre Arbogast Mndeme aliyefariki Aprili 12, 2018 na Michael Kiraghenja aliyefariki Aprili 11, 2018, wote wa jimbo hilo, ambapo Padre mmoja alikuwa anaumwa na alifariki katika hospitali ya KCMC, huku mapadre Wawili walifariki ghafla wakiwa usingizini.

Taarifa ya vifo vyao imetolewa jana na Askofu wa Jimbo la Same, Mhashamu Rogath Kimario.

Taarifa imesema kuwa haijawahi kutokea vifo vitatu vilivyopishana kwa saa 24 katika jimbo moja.

“Jana nilionana na Padri Kidavuri na alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda kuzika wenzie na nikampa pole pale St. Joseph, alikuwa mzima wa afya. Wapumzike kwa amani, amina,” alisema Padre Kimario.

Akithibitisha vifo hivyo jana, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Raymond Saba, alisema kanisa limepokea kwa mshtuko mkubwa kufuatia vifo hivyo vya ghafla.

“Vifo vimetushtua sana maana vimekuwa vya ghafla mno, tulikuwa nao na walikuwa wazima kabisa,” alisema Padre Saba.

Chelsea yaicharaza goli 3-2 Southampton
Urusi, Syria zaitaka Marekani isubiri matokeo ya mashambulizi