Shirika la usimamizi wa chakula na Dawa nchini Marekani (FDA) limeidhinisha chanjo ya ziada ya Pfizer kwa watu wenye umri wa  zaidi ya miaka 65 ikiwa wamepata chanjo yao ya mwisho angalau miezi sita iliyopita.

FDA limeidhinisha kwamba watu wazima wapo katika hatari kubwa ya kuugua sana na wanafanya kazi, kama wahudumu wa afya ni muhimu kupata chanjo ya ziada.

 “Wafanyakazi wanaotoa huduma za afya, walimu,wanaotunza watoto,  wanaouza vyakula na walio katika vituo vya wasio na makazi au magereza wanapaswa kuwa kwenye orodha hiyo,” Amesema kaimu kamishna wa FDA Janet Woodcock.

Hatahivyo, chanjo hizo bado zinahitaji idhini kutoka kwa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), inatarajiwa kuidhinisha hatua hiyo haraka baada ya mkutano wa Septemba 23.

Uamuzi wa jopo utajumuisha mapendekezo juu ya nani anastahili kupata chanjo ya ziada kwa misingi ya  ambaye yupo katika hatari zaidi, na wafanyikazi ambao wanaostahili kupata chanjo hiyo kwanza.

Hoja ya FDA ni ushindi kwa Rais Joe Biden, ambaye alikuwa ameahidi kuwa chanjo za ziada zitapatikana kuanzia mwezi huu ilimradi watapate idhini kutoka kwa shirika la FDA na kituo cha CDC.

Masijili wa vyama akutana na Jeshi la Polisi
Milioni 700 kukarabati barabara ya Karagwe