Marekani imefanya jaribio la kombora lake la masafa ya kati wiki kadhaa baada ya kujiondoa katika makubaliano muhimu na Urusi yaliyopiga marufuku silaha zenye uwezo kama huo za kinyuklia.

Marekani ilijiondoa katika makubaliano hayo mnamo tarehe 2 Agosti mwaka huu baada ya kuituhumu Urusi kwa kukiuka azimio hilo madai ambayo Moscow imeyakanusha

Pentagon imesema kuwa ilifanikiwa kurusha kombora hilo katika pwani ya California siku ya Jumapili, ambapo wachambuzi wanahofu kuwa kuanguka kwa makubaliano hayo kutazua ushindani wa utengenezaji wa silaha mpya za Nyuklia.

Aidha, makubaliano hayo yaliyo afikiwa katika kipindi cha vita baridi yalipiga marufuku silaha zenye uwezo wa kurushwa kati ya kilomita 500 hadi 5,500.

Pentagon imesema kuwa kombora hilo lililofyatuliwa kutoka kisiwa kinachodhibitiwa na wanamaji wa Marekani cha San Nicolas katika pwani ya Los Angeles, lilikuwa halina kichwa cha kinyuklia.

Hata hivyo, Silaha hiyo iliyofanyiwa majaribio haijafikia lengo lake la zaidi ya kilomita 500, kulingana na idara ya ulinzi nchini Marekani.

 

 

Kanda ya Ziwa yatajwa kuwa kinara wa matukio ya ukatili kwa watoto
MSD kujenga kituo cha mauzo na usambazaji dawa Simiyu