Marekani imesema kuwa haijafurahishwa na vitisho vilivyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif katika mkutano na Waziri mwenzake wa mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas jijini Tehran.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Morgan Ortagus amesema kuwa Iran inatakiwa kuchagua jibu moja tu rahisi, ijishushe iwe nchi ya kawaida au ikaidi ishuhudie uchumi wake utakavyosambaratika.

Aidha, Zarif aliituhumu Marekani kwa kufanya vita vya kiuchumi kutokana na vikwazo ilivyoiwekea Iran na akaonya kuwa wale wanaounga mkono vita wasitarajie kuwa salama.

Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas anataka kuyaokoa makubaliano ya nyuklia na Iran, lakini hakupiga hatua zozote za maana wakati wa ziara yake nchini humo. Maas alisema jana kuwa Ujerumani itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa mvutano hauongezeki kati ya Marekani na Iran.

Kampuni ya simu ya TECNO yatoa Ofa kwa wateja wake
Watoto milioni 108 duniani wanatumikishwa - FAO

Comments

comments