Marekani Jumatano imeweka vikwazo kwa watendaji 15 wa mafuta wa Sudan Kusini ambao imesema walikuwa chanzo muhimu cha fedha kwa serikali, hatua ambayo inalenga kuongeza shinikizo kwa rais wa Sudan, Salva Kiir kumaliza mgogoro na mzozo wa kibinadamu nchini kwake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters makampuni na taasisi za serikali huenda katika siku za mbeleni zikahitaji leseni maalum ya kufanya biashara nchini Marekani, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema.

Serikali ya Sudan Kusini na maafisa ambao ni wala rushwa, wanatumia mapato haya kununua silaha na kufadhili wanamgambo ambao wanadumaza amani, usalama na uthabiti nchini Sudan Kusini

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje imesema, Makundi yaliyo kwenye orodha yalihusika na harakati ambazo ni kinyume na sera za mambo ya nje na maslahi ya Marekani, kwa mujibu wa waraka uliochapishwa na wizara ya biashara ya Marekani Jumatano.

TCRA yaingilia kati mazungumzo ya Diamond dhidi ya Shonza
Meek Mill amkataa tena Jaji