Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson Masilingi amesema kuwa kitendo cha mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kuzunguka dunia nzima hakisaidii. BBC, Radio Ujerumani -DW, Sauti ya Amerika -VOA, kwasababu sio mahakama. hivyo anachofanya ni kuwachafua Watanzania na kuwavunjia heshima huku akijichafua yeye mwenyewe.

Ameyasema hayo jijini Washington DC wakati wa mahojiano maalumu na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili VOA, Mwamoyo Hamza ambapo amesema kuwa kuzunguka kote huko hakuwezi kumsaidia Lissu katika kutatua tatizo lake, hivyo amemshauri arudi nyumbani Tanzania ili asaidie upelelezi wa tukio hilo.

“Kutotambua kazi nzuri ya serikali ukazunguka dunia nzima unamtukana rais wako, vyombo vya dola, na kuwaambia Watanzania kwamba hamna haki nchini kwenu sio sawa,”amesema Masilingi

Aidha, kwa upande wke, Tundu Lissu amesema kuwa ni lazima kutofautisha kati ya serikali na taifa. huku akisema kuwa Serikali ya rais Magufuli sio taifa na inatakiwa kuongozwa na katiba.

Hata hivyo, Lissu amesema kuwa ataeleza juu ya matendo mabaya iwe yuko ndani ya Tanzania, au nje ya Tanzania au mahali popote anatimiza wajibu wake kama raia.

Mangula atua Njombe, anena kuhusu mauaji, 'Msijichukulie sheria mikononi'
Bunge lamjadili Lissu kusimamisha mshahara wake

Comments

comments