Mtendaji wa Mtaa wa Kyakailabwa Manispaa ya Bukoba Patrick Rwegasira (44) amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba akikabiliwa na mashtaka mawili ya kumtorosha mtoto mwenye umri wa miaka 14 na kumfanyia shambulio la aibu la kumpapasa matiti.

Wakili wa Serikali Joseph Mwakasege, mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Ruth Migan, amesema mshtakiwa Rwegasira baada ya kumtorosha mtoto huyo, aliishi naye kwake na alimpapasa matiti akilenga kumfanyia vitendo vya aibu.

Mwakasege amesema kuwa mshtakiwa huyo alimchukua mtoto huyo kutoka kwa wazazi wake Juni 2 hadi 04 mwaka huu alipokamatwa na kupelekwa Polisi.

Mshtakiwa amerejeshwa rumande kutokana na kukosa wadhamini na kesi yake itatajwa tena Julai 6 mwaka huu.

Rubondo MV kubeba watalii 50, magari 6
Mume wa Mercy akiri kumuua kwa spana ya bomba