Siku chache  baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya soka Tanzania bara  msimu wa 2015/16, Ratiba ya mwanzo ya michezo kadhaa  ya kirafiki ambayo kikosi cha Mbeya City Fc  kitacheza kwa ajili ya matayarisho ya msimu mpya wa 2016/17 imetoka.

Kwenye ratika hiyo, City  imepaga kucheza michezo mitatu ugenini, ambapo itaanza kwa kushuka dimbani Kamuzu Stadium jijini Blantyre Juni 18  kucheza na vigogo wa soka nchini Malawi, Big Bullets, ambapo kwa mujibu wa waandaaji, mchezo unatarajia kushuhudiwa na watazamaji wengi hasa ukizingatia ushawishi wa timu hiyo kwenye soka la nchi hiyo.

Mkuu kitengo cha habari na mawasiliano  kwenye kikosi cha City, Dismas Ten , amesema kuwa mchezo wa pili  nchini humo utachezwa jijini Lilongwe na utakuwa dhidi ya wenyeji Civo United, kwenye dimba la Civo Stadium hii itakuwa ni Juni  21.

“Baada ya mchezo huo  wa pili jijini Lilongwe,tutarudi kwenye mji  ulio kaskazini mwa nchi hiyo, Mzuzu, hapo tutacheza na wenyeji wetu Mzuni Fc, Juni 25 huu utakuwa mchezo wa mwisho kwenye ziara hii ya michezo ya kirafiki, baada ya hapo tutarudi nyumba tayari kwa michezo mingine ambayo  imepangwa ukiwemo  dhidi ya Simba tutakaocheza Morogoro”

RATIBA YA  MICHEZO YA MATAYARISHO YA MSIMU MPYA IKO HIVI:

  • JUNI 18 : Big Bullets Vs  City – KAMUZU Stadium. 16:00pm EAT.
  • JUNI 21: Civo United  Vs City – Civo Stadium.           16:00pm EAT.
  • JUNI 25: Mzuni FC  Vs  City – Mzuzu Stadium.          16:00pm EAT.
  • JULAI 31: City Vs Simba Sports- Jamhuri Stadium.  16:00pm EAT.

Kama mambo yatakwenda sawa, ratiba hii inaweza kuwa na ongezeko la  michezo miwili ya kirafiki katikati ya mwezi julai kabla ya mchezo wa mwisho wa mwezi huo dhidi ya Simba na mwingine  mwanzoni mwa mwezi wa nane kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu

Waziri Mkuu: Malikale zitumike kuondoa umasikini
Serikali ya Kenya yasaka majibu ya Odinga kuwaridhisha waandamanaji