Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa namna ilivyoipanga bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17.

Mbowe alitoa pongezi zake kwa Serikali baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kuwasilisha ukomo wa bajeti hiyo pamoja na mpango wa maendeleo kwa Mwaka mpya wa Fedha.

Mbowe alisema kuwa katika bajeti hiyo, Serikali imefanya mambo mema kwa kuelekeza kiaisi kikubwa kwa miradi ya maendeleo ya wananchi pamoja na kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi yasiyo ya lazima.

“Ukomo wa bajeti ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, hili nalo katika serikali ya awamu ya tano wameliona na kweli tuwaunge mkono, sio kila kitu tuone kibaya, cha msingi tuwape nafasi tuone watamalizaje huko mbele kwenye utekelezaji” Mbowe alisema.

Kadhalika, aliipongeza serikali kwa kupunguza kiasi cha utegemezi wa misaada katika bajeti ya mwaka mpya wa fedha kwa kuongeza matumizi ya fedha za ndani.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa NCCR – Mageuzi ambaye ni mbunge wa Vunjo, James Mbatia alikosoa mpango wa bajeti hiyo mpango wake hauna uhalisia kwani umelenga katika mapato ya muda mfupi yaliyopatikana kwa kukusanya mapato kutoka kwa watu waliokuwa wamekwepa kodi pamoja na faini.

Makala: Kagame alivyozika 'tofauti' na JK na kufufua Urafiki mzito na JPM (Picha)
Unywaji, uuzaji wa viroba wapigwa marufuku