Mchungaji wa kanisa la Pentekoste Kongwe, Kibaha mkoa wa Pwani Japhes Manwa (40) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumchoma moto mikononi na mgongoni mwanaye wa kiume mwenye umri wa miaka saba(7) ambaye ana ulemavu wa utindio wa ubongo.

Inadaiwa kuwa mchungaji huyo aliamua kumchoma mtoto wake moto kwa sababu hampendi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesi alisema kuwa tukio hilo lililipotiwa january 21 mwaka huu, ambapo amesema mtoto huyo mwenye ulemavu amabye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kalabaka alifanyiwa kitendo hicho cha kinyama kisa baba huyo hampendi.

”Mtoto huyo ni wa mwisho kati ya watoto wanne wa mtuhumiwa na mzazi mwenzake aitwaye Edna Esmail ambao hawaishi pamoja” amesema Kamanda Nyigesi.

Hata hivyo Ametoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto wanaotoa adhabu kali kwa watoto kama sehemu ya kuwakanya madhara yake huwa ni makubwa.

Aidha kamanda huyo amekemea vitendo vya kunyanyapaa watoto wenye ulemavu kwani wao ni watoto kama watoto wengine ndani ya familia.

Kliniki tembezi yanufaisha watanzania 200 Kiteto
Tanzania kinara zao la nazi Afrika