Mshambuliaji wa mabingwa wa soka Tanzania bara Simba Meddie Kagere ametaja siri ya mafanikio yake ni kujituma, kushirikiana vizuri na wenzake na kuhakikisha kila siku anakuwa bora kwa kufanya mazoezi.

Msimu uliopita, Kagere aliibuka mfungaji bora wa VPL baada ya kufunga mabao 23, na msimu huu msimu huu tayari ameshafunga mabao 19 na ni wazi anaelekea kuwa mfungaji bora kwa msimu wa pili mfululizo.

Nyota huyo raia wa Rwanda amesema anachofanya kila siku ni kuhakikisha anakuwa bora kuliko wachezaji wazawa kwani anaamini dhumuni la yeye kusajiliwa na Simba ni pamoja na kuonyesha kuwa ana kitu zaidi ya wachezaji wa ndani.

“Ukiwa mchezaji wa kigeni lazima uonyeshe utofauti na wachezaji wa ndani na Hivyo mimi huwa najituma zaidi ili kuhakikisha nakuwa bora wakati wote. Jambo moja kubwa huwa nahakikisha sipati majeraha ya mara kwa mara na nakuwa na mwendelezo mzuri wa kufunga kila msimu.” Amesema Kagere.

Kagere kwa sasa yuko kwao Rwanda na familia yake wakati huu mapumziko ya kudhibiti maambukizo ya virusi vya Corona.

Uingereza: mvulana wa miaka 13 afariki dunia kwa Covid 19
Wagonjwa wawili wa Covid 19 wathibitika Burundi

Comments

comments