Klabu ya Mediama ya nchini Ghana imesitisha mkataba wa aliye kuwa beki wake raia wa Ivory coast Zana Oumary Coulbaly kwa makubaliano ya pande zote mbili,

Beki huyo wa zamani wa klabu za Asec Mimos, African Sports, As Vita na klabu ya Simba SC ya Tanzania alijiungiunga na klabu hiyo August 2020 akitokea As Vita kwa usajili huru.

Katika msimu ulioisha Coulbaly ameichezea Mediama mechi mbili tu za ligi kuu ya Ghana tangu ajiunge na klabu hiyo.

Alicheza dakika 90 katika mechi dhidi ya Great Olympic na dakika 58 katika mechi dhidi ya Ashant Gold SC.

Simba SC yajitoa Kagame Cup 2021
Mauya amtaja Mukoko kipigo cha Kigoma