Rapa Meek Mill aonyesha kuchukizwa na kuamua kuivunjia ukimya Label inayosimamia kazi zake kwa kinachodaiwa kuwa Lebal hiyo haijamlipa pesa zilizotikana na kuuzwa kwa muziki wake.

Meek Mill amevunja ukimya kuhusu sakata hilo siku ya jumatatu oktoba 25,2020. kupitia ukarasa wake wa mtandao wa Twitter kwa kuandika kwenye post kadhaa maneno yenye kudhihirisha kuchukizwa na kinachoendelea kati yake na Lebal hiyo.

“Sijalipwa pesa zangu kwenye muziki na mpaka sasa sifahamu ni kiasi gani cha pesa Label imeingiza kutoka kwenye muziki wangu, ninahitaji Mwanasheria haraka iwezekanavyo.” Ameandika Mill.

Licha ya ujumbe huo Meek Mill ametishia kuweka wazi mkataba wake na Lebal hiyo kama hatoona majibu yeyote mpaka itakapofika jumatatu ya wiki ijayo Nov 1, 2021 kwa madai ya kutaka kuambia Dunia juu ya uozo unaofanywa na Lebal hiyo.

Licha ya yote hayo, rapa huyo hajaweka wazi Lebal anayoituhumu kati Maybach Music, Rock Nation pamoja na Atlanta Records.

Rayvann achukizwa na chuki za wasanii Tanzania.
Mwanamke aliyejifungua watoto 9 awaonyesha sura zao