Wiki iliyopita muigizaji kutoka kiwanda cha bongo movie Wema Sepetu alifunguka kwamba aliyekuwa Meneja wa wasanii wake Petitiman Wakuache ndie aliyekwamisha wasanii wa Endless Fame kutofanya vizuri  kutokana na usimamizi mbovu.

Mirror pamoja na Alli Luna ni wasanii ambao walitarajiwa kuja kufanya vizuri katika soko la muziki wa bongo fleva lakini ikawa kinyume chake na ndio sababu ya Madam Sepetu kuamua kurudisha lawama kwenye menejiment aliyoikabidhi.

Petitiman hakua nyuma kujibu tuhuma ambazo alielekezewa na aliyekuwa bosi wake wa zamani kabla ya kuanzisha lebo yake binafsi ya LFLG inayowasimamia wasanii Nuh Mziwanda pamoja na Billnass ambao kwa  sasa wanafanya poa.

Hata hivyo amesema ya kuwa kabla menejiment kukufiksha mbali msanii mwenyewe anatakiwa kujituma huku akiongeza kwamba kwa sasa kazi yake ndio itatoa majibu ya kama yeye ndo alikuwa kikwazo Endless Fame. Msikilize hapa chini

Raisi Magufuli;Wafanyakazi Wa jeshi la Polisi Wasiokua Askari Wahamishiwe Utumishi
Mbeya City FC Yamnasa Rajab Zahir