Siku chache baada ya rapa Young Dee na aliyekuwa maneja wake, Max kuwekana kando kibiashara, meneja huyo amezungumzia kile kinachozungumzwa kwenye mitandao kuwa rapa huyo amerudia kubwia unga.

Tetesi hizi ziliibuka hivi karibuni ikiwa ni miezi michache imepita tangu Young Dee alipojitokeza hadharani kukiri kuwa alikuwa anatumia dawa za kulevya na kwamba alikuwa ameachana nayo na kuamua kufanya kazi tena na meneja wake huyo, Max.

Akifunguka kupitia FNL ya East Africa Radio, Max alieleza kuwa yeye pia amekuwa akisikia tetesi hizo kama ambavyo alikuwa akisikia awali kabla ya rapa huyo kukiri kwake.

“I hear things; I have no proof or evidence (nimekuwa nikisia mambo, sina vielelezo. Lakini hata mwanzo nilikuwa nasikia vitu, na nikiuliza naambiwa sio. Lakini tena hii story ni ileile inarudi. Lakini siwezi hata siku moja kusema nimemkuta Young Dee anatumia unga, sijawahi kumuona,”alisema Max.

Max alisema kuwa aliamua kumuomba rapa huyo kuondoka nyumbani kwake alipokuwa akiishi kutokana na kile alichodai ni utovu wa nidhamu.

Hata hivyo, alieleza kuwa yeye na rapa huyo walikuwa wanapendana sana hadi kufikia hatua ya kuitana majina ya utani, “alikuwa ananiita mimi Daddy, Lucius (muigizaji wa Empire), na mimi nilikuwa namuita Hasheem (rapa muigizaji wa Empire kama mtoto wa Lucius).

Lionel Messi Anyimwa Ruhusa
Ubishi Wa Nani Mkali Kumalizwa Leo