Mshambuliaji mpya wa klabu ya Girondins de Bordeaux ya nchini Ufaransa, Jeremy Menez amelazimika kufanyia upasuaji baada ya kupata majeraha ya sikio wakati akiwa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya FC Lorient hapo jana.

Menez ambaye alijiunga na klabu hiyo mwanzoni mwa juma hili akitokea nchini Italia alipokua akiitumikia klabu ya AC Milan, alipata majeraha ya sikio lake la upande wa kulia, baada ya kukanyagwa kwa bahati mbaya na kiungo wa FC Lorient, Didier Ndong dakika 15 baada ya kuingia uwanjani.

Jeremy Menez after his savage injury

Kitendo hicho kilimsababishia maumivu makali mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, na uchunguzi wa awali uliofanywa uwanjani hapo ulibaini kipande cha nyama ya sikio lake kiling’oka.

“Jeremy alifanyiwa upasuiaji mdogo kutokana na jareha lililomkabili katika mchezo wa jana, na sasa anaendelea vyema,” imeeleza taarifa iliyotolewa na klabu ya Bordeaux.

Hii inakua bahati mbaya kwa Menez, kutokana na majeraha kumuandama kwa mara ya pili mfululizo, kwani msimu uliopita alikosa sehemu kubwa ya ligi ya nchini Italia, kutokana na maumivu ya mgongo.

Rummenigge: Man Utd Wameshindwa Kumtumia Schweinsteiger
Video: Taarifa kuhusu Rais wa Simba Aveva na wenzake watatu kushikiliwa na Polisi