Beki wa Coastal Union, Miraj Adam aliyefunga mabao katika mechi zote timu yake ikishinda 2-0 dhidi ya Yanga na 1-0 dhidi ya Azam FC, hataruhusiwa kucheza keshokutwa dhidi ya Simba.

Miraj aliyefunga bao la kwanza dhidi ya Yanga na bao pekee dhidi ya Azam, yote kwa mipira ya adhabu amezuiwa kucheza dhidi ya Simba katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumamosi.

Na sababu ni kwamba Miraj ni mchezaji anayecheza kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu Coastal Union kutoka Simba, hivyo makubaliano baina ya timu hizo yamemkwamisha kucheza siku hiyo.

Kocha Ally Jangalu wa Coastal Union amesema kwamba ni pigo kumkosa Miraj katika mchezo muhimu kama huo, lakini atawatumia wachezaji wengine.

“Tuna wachezaji wengi vijana wadogo, wenye morali na nitaangalia mmoja kati yao atachukua nafasi ya Miraj, ambaye bahati nzuri tutamkosa kwa mchezo huu mmoja tu,”amesema.

Simba Kujenga Uwanja Kwa Fedha Za Emmanuel Okwi
UVCCM Wamkataa Balozi Mwapachu, wadai ana dhambi ya usaliti