Mke wa msanii wa muziki nchini Bi Amina amesema mara ya kwanza kuonana na mume wake Alikiba ilikuwa kwenye ndege.

Watu wengi wamekuwa na hamu ya kumjua kiundani mke wa Alikiba ambaye ni mwenyeji wa Mombasa, leo hii amefunguka hayo katika kituo kimoja cha habari nchini na ameweka wazi kuwa hatumii mtandao wa kijamii wa instagram kwani tayari kuna kurasa mbalimbali zimefunguliwa zikitumia jina lake.

Katika mahojiano aliyofanyiwa pamoja na mume wake Alikiba ameshindwa kujibu swali aliloulizwa likimtaka aseme kama atakuwa tayari endapo mumewe Alikiba akihitaji kuongeza mke mwingine ambapo Alikiba alionesha utayari wa jambo hilo endapo akipewa nafasi hiyo.

Amina amemaliza shahada ya kwanza kitivo cha mambo ya fedha huko nchini Nairobi, amehitimu masomo yake mwaka 2016.

Ameongezea kuwa Alikiba alimfahamu kupitia Binamu yake wa kiume ambaye alikuwa mtu wake wa karibu sana na Msanii huyo na wamekuwa marafiki kwa muda mpaka pale Mfalme Kiba alipomtamkia anampenda na kumshauri aende kujitambulisha kwa  wazazi wake.

Aidha Bi Amina ni mototo wa mwisho kwenye familia ya watoto watano.

Ali Kiba afunguka kufikishwa mahakamani akidaiwa matunzo ya mtoto 
Leo kumbukumbu ya miaka 37 kifo cha Bob Marley

Comments

comments