Mkenya Eliud Kipchoge amefanikiwa kujinyakulia medali ya dhahabu mara baada ya kuwaacha wapinzani wake  kwa muda mrefu  katika mbio za marathon upande wa wanaume katika michezo ya Olimpiki inayofanyika  Rio de Janeiro nchini brazil.

Kipchoge mwenye umri wa miaka 31 ambaye pia  ni mshindi wa mbio za London Marathon  mwezi Aprili amefanikiwa kumaliza mbio hizo katika muda wa masaa mawili na dakika nane na sekunde 44.

Feyisa Lilesa wa Ethiopia alimaliza wa pili akiwa nyuma ya Kipchoge kwa sekunde 70 ili kushinda fedha, na nafasi ya tatu imechukuliwa na  raia wa Marekani Galen Rupp aliyejishindia medali ya shaba.

Ushindi huo sasa unaipatia kenya medali yake ya sita kabla ya kukamilika kwa michezo hiyo siku ya Jumapili.

Kenya pia ilijishindia medali ya dhahabu katika mbio za marathon upande wa wanawake katika siku ya kwanza ya mashindano hayo ambapo Jemimah Sumgong aliibuka mshindi

Lipumba aipasua rasmi CUF, Vurugu zaibuka Mkutano Mkuu
Watu 30 Wauawa Na Wengine 90 Wajeruhiwa Nchini Uturuki