Wakulima wa mazao mbalimbali wilayani Njombe Mkoani Njombe wameacha kutumia dawa za madukani zenye kemikali za kuulia wadudu, kukuzia pamoja na mbolea, badala yake wanatumia mkojo wa Sungura ili kukabiliana na changamoto zinazokabili mazao yao.

Wakizungumza na waandishi wa habari wakulima hao wanasema kuwa wamefanya majaribio katika mazao yao na kubaini kuwa mkojo wa Sungura unaweza kutumika kama mbolea ya kukuzia pamoja na dawa ya kuulia wadudu.

Aidha, mmoja wa wakulima hao anayejulikana kwa jina la Obeid Changula amesema kuwa baada ya kusikia kwa baadhi ya wakulima waliojaribu matumizi ya mkojo huo ilimlazimu kufanya majaribio katika mazao yake ikiwemo mahindi na kubaini ukweli huo na hivyo hawatumii dawa zenye kemikali kuendeshea Kilimo chao.

“Nilivyosikia nilifanya majaribio shambani kwangu ambako mahindi yangu yalikuwa yameanza kushambuliwa na wadudu kwani yalikua yamedhoofu,wadudu walikua wameanza kula chini ya mizizi hivyo basi nikachukua mkojo wa Sungura na kuchanganya na maji,”amesema Changula

Hata hivyo, ameongeza kuwa baada ya kunyunyuzia katika mahindi yake yalibadilika na kuwa yenye ubora na kubaini kuwa mkojo huo ni mbolea licha ya kuua wadudu lakini pia inakuza mazao.

 

 

Vijana mkoani Njombe watakiwa kuunda vikundi
Bocco, Okwi wasafisha njia ya Ubingwa 2017/18

Comments

comments