Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera anajipanga kuirudisha timu ya Tanzania Prisons mkoani humo, baada ya kuhamia Uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa.

Mh. Homera amesema.mpaka sasa hafahamu sababu zilizopelekea timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza kwa nini ilihamia mkoani Rukwa.

Amesema anaendelea kuzungumza na viongozi wa Tanzania Prisons ili kujua sababu, kisha atafanya ushawishi ili kuirudisha Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

“Tunataka Tanzania Prisons irudi Mbeya, kwa sababu hadi sasa bado sijafahamu sababu zilizopelekea kuhama Mbeya”.

“Ninaendelea na mazungumzo na viongozi wa Tanzania Prisons ili kujua sababu zilizowahamisha hapa, kisha nitajitahidi kuwashawishi ili warudi Mbeya.” amesema Homera.

Tanzania Prisons ilihamia Uwanja wa Nelson Mandela msimu wa 2020/21 na michezo yote ya nyumbani ilicheza kwenye uwanja huo.

Endapo itaridhia kurudi Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, itaungana na timu za Mbeya City na Mbeya Kwanza zitakazotumia Uwanja huo msimu ujao.

Serikali ya Zanzibar yaapa kuulinda Muungano
Yametimia, Azam FC yamalizana na Mbombo