Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo (CDF) amesema majeshi yamejipanga kukabiliana na vitendo vya uchochezi vinavyohatarisha usalama wa nchi.

Jenerali Mabeyo ametoa kauli hiyo leo tarehe 13 Aprili 2019, wakati akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Rais, Chamwino jijini Dodoma.

“Tunaendelea kufuatila kauli tata zenye kuashiria ishara za uchochezi ndani ya nchi yetu, tuko tayari kukabiliana na vitendo vyovyote vitakavyotokana na uchochezi huo,” amesema Jenerali Mabeyo.

Aidha Jenerali Mabeyo amezungumzia migogoro inayoendelea katika baadhi ya nchi jirani, akisema kwamba jeshi liko tayari kuliinda nchi endapo migogoro hiyo itaathiri kwa namna yoyote ile Tanzania.

“Migogoro inayofukuta katika nchi jirani inaweza ika (influence ) kuleta hali isiyotabirika katika nchi yetu, nikuhakikishie mheshimiwa (Rais John Magufuli)tuko tayari kuilinda nchi yetu.

“Kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama tuko tayari kulinda wananchi na mali zao, na tuko mstari wa mbele kushirikiana na wenzetu ” amesema Jenerali  Mabeyo.

 

Wananchi wafunga ofisi za serikali ya kata
CAG: Kuna upungufu wa mabasi 165 ya mwendo kasi

Comments

comments