Aliyekua Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting Cherles Boniface Mkwasa amefunguka kwa undani kilichopelekea kujiuzulu kukinoa kikosi cha Klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23.

Mkwasa alifikia maamuzi ya kuondoka klabuni hapo jana Jumatatu (Desemba 05), na baadae Uongozi kuthibitisha safari yake ya kujiweka pembeni na kumwachia Kocha mwingine ambaye aliamini huenda akawa na bahati ya kuinusuru Ruvu Shooting.

Kocha huyo mzawa amesema, ililazimika kujiuzulu kwa sababu amekua na historia nzuri na Klabu ya Ruvu Shooting, ambayo amekiri kuipenda na kuithamini, hivyo aliona kuna haja ya heshima yake kusalia klabuni hapo kwa maamuzi ya kujiuzu.

Hata hivyo Mkwasa amesema kabla ya kuwasilisha barua kwa Uongozi, alikutana na Wachezaji wake wote na kuwaeleza nia yake ya kujiuzulu, na kwa bahati nzuri kila mmoja alimuelewa.

“Kwa mwenendo wa timu niliona ni heri niake pembeni kwa kuwa Ruvu Shooting ni Klabu yangu na ninaipenda na kuiheshimu, hivyo niliona mambo yasiwe mengi, kwa kulinda heshima yangu na ya klabu pia,”

“Nilikuwa nimeshaongea na Wachezaji wangu kwa kuwaambia jambo la mimi kuondoka, nilichokifanya baadae ni kuwasilisha Barua kwa viongozi wa juu kuwafahamisha kujiuzulu kwangu, ndivyo ilivyokuwa,” amesema Mkwasa

Tayari Uongozi wa Ruvu Shooting kupitia Idara yake ya Habari na Mawasilino leo Jumanne (Desemba 05), imemtangaza Kocha Mbwana Makata kuwa mbadala wa Charles Boniface Mkwasa.

Bidhaa zaidi ya 8000 za Tanzania kuuzwa China
Nelson Okwa aweka wazi hatma yake Simba SC