Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema wamempokea kwa mikono miwili mpinzani wao MC Alger ya Algeria, katika michuano ya kombe la shirikisho.

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), limeipangia Yanga kucheza na timu hiyo katika michuano ya Kombe la Shirikisho katika droo iliyofanyika jana mchana mjini Cairo nchini Misri.

“Tumeona kuhusiana na kupangwa na timu hiyo. Tumefika hatua hii tulitarajia kupangwa na timu yoyote.

“Hivyo hatuna sababu ya kusema tumeshituka sana, tunajua kuna ugumu na muhimu ni maandalizi ya kutosha,” Alisema Mkwasa.

Katibu huyo ambaye kitaaluma ni kocha, alikiri Yanga imekuwa katika wakati mgumu kifedha, lakini imekuwa ikijitahidi kufanya kila linalowezekana ili mambo yaende safi.

Michy Batshuayi Kubaki London
Paris Saint-Germain Wasubiri Jibu La Arsene Wenger