Msanii wa kizazi kipya kutoka Dodoma, Moni wa Centrol zone amejibu tuhuma zinazomkabili za kuiba wazo la wimbo wake wa ‘Matango Pori’ kutoka kwenye wimbo wa ‘Matango Nyanya’ wa H Mbizo.

Moni ambaye hivi sasa anavimbisha misuli kwenye vyombo vya habari na mitaani kutokana na ukubwa wa ‘Matango Pori’, amekana tuhuma hizo na kueleza kuwa kilichofanana kwenye nyimbo hizo ni maneno machache tu na sio wazo zima na uandishi.

Akizungumza na E-news ya EATV, Moni amesema hakuna ukweli kuhusu kuiba wazo la wimbo huo.

“Kwanza mimi naona huu ni msaada kwa H Mbizo kwasabubu watu wanapozungumzia wimbo wangu wanazungumzia na wimbo wake,” alisema.

“H Mbizo ni kaka yangu lakini hajawahi kunishawishi mimi kufanya muziki mpaka kufikia hatua ya kumuibia wazo la wimbo au hata wimbo mzima,” aliongeza.

Hivi karibuni, H Mbizo alikaririwa akimtupia lawama Moni kwa kutumia wazo la wimbo wake ambao aliutoa miaka miwili iliyopita bila kumpa taarifa, kitendo alichokitafsiri kama ni kurudishana nyuma kwenye tasnia ya sanaa.

Mabilioni ya Escrow yaliyotoroshwa sasa kurejeshwa nchini
Mbowe azidi kuweweseka na madiwani waliohama chama