Mzunguuko wa tano wa michuano ya kombe la ligi nchini England (EFL Cup) ulihitimishwa rasmi usiku wa kuamkia hii leo kwa michezo mitatu kuchezwa.

Man Utd ambao walikua nyumbani Old Trafford waliwakabili mahasimu wao Man city na kufanikiwa kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Bao hilo la Man Utd lilikwamishwa wavuni na kiungo mshambuliaji kutoka nchini Hispania Juan Mata.

Chelsea walifunga safari hadi London Stadium kucheza na wenyeji wao West Ham Utd ambao walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Mabao ya wenyeji yalifungwa na Cheikhou Kouyate pamoja na Edimilson Fernandes huku Gary Cahill akiwapoza The Blues kwa kufunga bao la kufutia machozi.

Mchezo mwingine wa michuano hiyo uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo ulishuhudia Southampton wakiwa nyumbani St Mary’s Stadium, wakipapatuana na Sunderland.

Mpaka dakika 90 za mchezo huo zinamalizika The Saints walichomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri kupitia kwa Sofiane Boufal.

Erick Thohir: Bado Tunaamini Kwa Frank de Boer
Video: Jeshi la Polisi Dar lawashikilia wachina kwa utekaji, lakusanya Sh. mil. 6.9 kwa siku 7