Kocha mpya wa Manchester United, Jose Mourinho ameanza kwa kasi kazi yake mpya akianza kubadili kila kitu kilichokuwa kikitumika kama miungu ya mtangulizi wake Louis Van Gaal kuwahakiki wachezaji tangu wanapokuwa katika mazoezi.

Moja kati ya mabadiliko makubwa aliyoyafanya Mourinho ni kuondoa kamera zote zilizokuwa katika uwanja wa mazoezi wa Carrington.

Kamera hizo zilikuwa zinatumiwa na mtangulizi wake kama ‘hirizi’ ya kuwapa morali zaidi wachezaji kufanya mazoezi kadri inavyotakiwa kwani baada ya muda hukaa na kupitia matukio yote yaliyokuwa yanaendelea uwanjani. Aliamini hiyo ingemsaidia kuhakikisha hakuna anayetegea mazoezini.

Hata hivyo, kamera hizo zilikuwa zinawachukiza wachezaji wengi ambao walikuwa wanazichukulia kama kifaa kinachotumiwa na Van Gaal kuwachunguza, kuingilia uhuru wao.

Mourinho, kama Meneja wa timu hiyo ameamuru kamera zote ziondolewe kwa sababu haitaji kamera kumueleza kile alichokiona kwa macho yake (kwani huwa uwanjani muda huo). Uamuzi huo umepokelewa kwa shangwe kubwa na wachezaji wa Manchester United.

Mourinho

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu kutoka katika uwanja huo wa Mazoezi kilichoongea na The Mirror, wachezaji sasa wamepata morali zaidi kwani Mourinho anawaweka karibu tofauti na Van Gaal ambaye uhusiano wake ulikuwa kama wanafunzi wa shule ya msingi na mwalimu wao.

Inadaiwa kuwa mkogwe wa soka, Michael Carrick maarufu kama ‘fundi’ ameeleza kuwa anatamani angerudi nyuma awe na miaka 25 ili aweze kufaidi zaidi matunda ya malezi ya Mourinho.

Katika hatua nyingine, Mourinho ambaye awali jina lake la ‘msema hovyo’ lilichukua nafasi kubwa zaidi amepachikwa jina lingine jipya la heshima la ‘Mr Meticulous’ yaani ‘Mtu Makini’.

 

 

Makala: Marufuku ya mikutano ya hadhara haiathiri ‘nguvu ya Lowassa’
Neymar: Bila Messi hakuna Soka